loader

Sera ya Faragha

Tarehe ya mwisho ya mabadiliko: Agosti 16, 2022

Toleo la sasa: 1.2

Amo Inc. (kama inavorejelewa hapa kwa jina lake la kazi "Twenzao" na "Huduma" ni mmiliki pekee wa taarifa zinazokusanywa kupitia huduma hii. Hatutauza, kushea au kukodisha kwa watu wengine katika njia tofauti na hizi zilizobainishwa katika taarifa hii.

Usajili

Ili kutumia Twenzao, Mwanachama anapaswa kwanza kujaza fomu au nakala yetu ya usajili. Katika kipindi cha usajili mwanachama anaweza kuhitajika kutoa taarifa zake za mawasiliano yaani jina na barua pepe. Taarifa hizi zitatumika kwa ajili ya uthibitisho na kuwasiliana na mwanachama kuhusiana na huduma ya Twenzao ambayo ameonyesha nia au dhamira ya kuitumia. Kujisajili kwenye huduma ya Twenzao itahesabika mwanachama ameridhia taarifa zake kutumika kama ilivoelezwa hapo juu.

Vidakuzi ("Cookies")

Vidakuzi au "cookies" ni taarifa fupi ambayo imetunzwa kwenye kiendeshi diski kuu ya mwanachama yenye taarifa zake husika. Matumizi ya vidakuzi kwa namna yoyote ile hayaunganishwi na mtu yeyote kwa taarifa yoyote ambayo imetambulika wakati akitumia tovuti yetu. Mathalani kwa kuweka vidakuzi katika huduma ya Twenzao, mwanachama hatahitajika kuweka nywila zaidi ya mara moja, kwa hivyo ataokoa muda akiwa kwenye huduma yetu. Kama mwanachama hatokubaliana na matumizi ya vidakuzi, bado anaweza kutumia Twenzao. Hasara iliyopo kwa hili ni kwamba mwamachama huyo atakuwa amebanwa kwenye baadhi ya maeneo ya huduma zetu. Vidakuzi vinaweza kutusaidia kufuatilia na kupata shauku ya mwanachama wetu kukuza ujuzi wa huduma yetu.

Ulinzi

Twenzao inachukua kila tahadhari kulinda taarifa za wanachama wetu. Kama una swali lolote kuhusiana na ulinzi wa huduma zetu, tafadhali wasiliana nasi.

Usalama na Utii wa Sheria

Twenzao inaweza kutoa taarifa zako kwenye mahakama, watekelezaji wa sheria, au mamlaka za serikali, au kuruhusu mhusika wa tatu kwa namna ambavyo tunatakiwa kufanya kwa mujibu wa sheria ya Tanzania au kama utolewaji wa taarifa ni muhimu,

  1. Kutii matakwa ya kisheria na kujibu malalamiko yaliyowekwa dhidi ya Twenzao,
  2. kujibu maombi yaliyo thibitishwa yanayohusiana na uchunguzi wa kijinai unaodhaniwa au kutuhumiwa shughuli zilizo kinyume cha sheria au kazi yoyote ile ambayo inaweza kutufanya sisi, wewe au mtu yeyote yule kati ya watumiaji wa huduma zetu kuwajibika kisheria,
  3. kutekeleza na kusimamia mashariti yetu ya huduma au makubaliano mengine na wanachama,
  4. kwa uchunguzi wa ulaghai na uzuiaji wake, tahtmini ya hatari, msaada wa wateja, maendeleo ya bidhaa na sababu za utatuzi, au
  5. kulinda haki, mali au usalama binafsi wa Twenzao, wafanyakazi wake, wanachama na wamachama wengine katika jamii.

 

Tutajaribu kuwapa taarifa watumiaji wa huduma zetu kuhusiana na maombi ya namna hii isipokuwa:

  1. Kama kutoa taarifa kunazuiwa na utaratibu wa kisheria, tunapokea kwa amri ya mahakama au kwa sheria inayotumika, au
  2. Tunaamini kwamba kutoa taarifa sio mbinu sahihi, kutaleta hatari ya maumivu ya kimwili kwa yeyote au kikundi, au kutengeneza au kuongeza hatari ya udanganyifu katika mali za Twenzao, mwanachama wake, na huduma kwa ujumla wake.

Kwenye mazingira ambayo itatubidi kufuata maombi ya kisheria bila kutoa taarifa kwa sababu hizi, tutajaribu kumpa taarifa mwanachama wetu kuhusiana na ombi hilo, baada ya ukweli kwamba kama tukiamua kwa nia njema kwamba hatuzuiwi kwa mujibu wa sheria kufanya hivyo na hakuna hatari yoyote ile itakayotokea.

 

Taarifa zinazokusanywa

Mtu anapojisajili anatoa taarifa mbalimbali kumhusu, kama vile majina yake, barua pepe na nambari ya simu. Vile vile, tunatumia anuani za IP kufuatilia mienendo ya wanachama na kukusanya taarifa nyinginezo za watumiaji ili kuendelea kuboresha Huduma na kusimamia usalama wa watumiaji wote pamoja na Huduma yenyewe. Kwa kuendelea kutumia Huduma, mtumiaji anaridhia ukusanyaji huu wa taarifa zake.

Mawasiliano na Mwanachama

Tutakuwa tukituma taarifa kuhusu Huduma kupitia njia mbalimbali kama vile simu, barua pepe, SMS, taarifa za ndani ya app (push notifications) na mitandao ya kijamii. Kwa kutumia app ya Twenzao, mtumiaji anaridhia kuwa taarifa zake zinaweza kurekodiwa kwa sababu za kiusalama na kuboresha utoaji wa Huduma, na Twenzao haihitaji ridhaa ya ziada kutoka kwa mtumiaji kila ukusanyaji huu wa taarifa unapojitokeza.

Kujiondoa Kwenye Upokeaji wa Taarifa

Mwanachama ambaye hatopenda kuendelea kupokea jarida zetu anaweza kuchagua kutokupokea mawasiliano yetu kwa kuchagua kujiondoa kupokea taarifa kwa njia ya barua pepe.

Kusitisha Uanachama na Kufuta Taarifa

Wakati wowote ule mwanachama anaweza kufuta akaunti yake ya Twenzao kwa kwenda kwenye Wasifu > Mipangilio ya Akaunti > Futa Akaunti au kwa kuwasiliana nasi. Katika hatua hii akaunti tajwa itawekewa alama ya kutokufanya kazi ha hatimaye kufutwa kabisa ndani ya kipindi fulani. Katika kipindi hicho mwanachama anaweza kuhuisha akaunti yake iwapo atapenda.

Endapo Mwanachama hatahuisha akaunti yake, taarifa zake zote zitafutwa milele kutoka kwenye mfumo wa Twenzao pale ambapo akaunti yake itafutwa. Hivyo basi, kusitisha uanachama ndiyo namna pia ya kuomba kufutwa kwa taarifa za Mwanachama.

Taarifa za Mabadiliko

Kama tutafanya mabadiliko katika sera yetu ya faragha, tutatoa taarifa kwa wanachama wetu wote kupitia barua pepe na katika ukurasa huu ili wafahamu ni taarifa zipi tunakusanya, namna gani tunazitumia na katika mazingira gani. Taarifa kuhusu Mwanachama tunazozikusanya tutazitumia kulingana na sera ya faragha husika wakati wa ukusanyaji wa taarifa hizo.